“Mtazamo Mpya wa Kusaidia Biashara Kukua Kwa Maarifa, Ushauri na Zana Halisi”
Wajasiriamali Smart Clinic ni jukwaa la kipekee lililoanzishwa na Kreative Karakana kwa ajili ya kuwasaidia wajasiriamali wa Kitanzania kukabiliana na changamoto halisi zinazowakabili katika kuanzisha, kuendesha, na kukuza biashara zao. Clinic hii ni mahali ambapo wajasiriamali hukutana ana kwa ana na wataalamu wa biashara kwa ushauri, uchunguzi wa changamoto, maarifa ya kitaalamu, na suluhisho la moja kwa moja.
Tofauti na semina au mafunzo ya kawaida, Smart Clinic inalenga kuwa mahali pa kutatua matatizo moja kwa moja iwe ni kuhusu mitaji, wateja, mikakati ya masoko, mipango ya kifedha au usimamizi wa biashara. Lengo ni kuhakikisha kila mshiriki anaondoka na hatua ya kuchukua, msaada wa kiutendaji, na mwelekeo mpya wa biashara yake.
Tumegundua kuwa changamoto nyingi zinazowakumba wajasiriamali hazitatuliwi kwa ushauri wa jumla. Biashara nyingi zina matatizo yanayohitaji muda, uelewa wa ndani, na msaada wa karibu ili kuyatatua. Kupitia Smart Clinic, tunawapatia wajasiriamali muda wa kuketi na wataalamu, kuelezea changamoto zao moja kwa moja, na kupata mwongozo unaozingatia mazingira yao halisi.
Hii ni sehemu ya dhamira ya Kreative Karakana ya kubadilisha mwelekeo wa ujasiriamali Tanzania kutoka bahati na majaribio, kwenda maarifa, mbinu, na msaada wa kweli. Smart Clinic ni sehemu ya mfumo mzima tunaoujenga kupitia Karakana Learning na Kreative Huduma, unaowapa wajasiriamali maarifa, huduma za kidigitali, na nyenzo za kuendeleza biashara zao.
Toleo la kwanza la Wajasiriamali Smart Clinic lilifanyika mwezi Machi 2025 na lilihudhuriwa na wajasiriamali 20 waliopatikana kupitia mchakato wa maombi na uchunguzi wa mahitaji yao. Toleo hili lilijikita katika changamoto kubwa inayowakumba wengi: mtaji.
Ndiyo maana tuliandaa kliniki hii tukiongozwa na kaulimbiu:
“Njia Rahisi ya Kupata Mtaji wa Biashara Yako!”
Bila kutaja moja kwa moja kuwa tunazungumzia VICOBA, tulitaka kuchokoza fikra na kuibua mjadala halisi.
Katika kikao hicho, tuliambatana na uzinduzi rasmi wa kozi ya kwanza kabisa ya Karakana Learning –
“VICOBA na Maendeleo”
Kozi hii ilifundishwa na mtaalamu mashuhuri Yanga Omary, ambaye ni mwalimu wa VICOBA na kiongozi mwenye uzoefu mkubwa katika kusaidia vikundi vya kijamii na kiuchumi.
Wajasiriamali walipata fursa ya:
Kujifunza mbinu sahihi za kutumia VICOBA kama chanzo salama na endelevu cha mtaji.
Kufahamu jinsi ya kuendesha vikundi kwa uwajibikaji, uwazi, na malengo ya kweli ya kimaendeleo.
Kujadili changamoto wanazopitia na kupata majibu ya moja kwa moja kutoka kwa wakufunzi na wataalamu.
Kujisajili kwenye Karakana Learning Platform kwa ajili ya kuendelea na mafunzo na kupata msaada hata baada ya kliniki.
Je, unataka kujua jinsi ya kutumia VICOBA kama chanzo halali na endelevu cha mtaji? Ungependa kuelewa mbinu sahihi za uendeshaji wa kikundi, uwajibikaji, na nidhamu ya kifedha inayoleta maendeleo ya kweli?
Ipe biashara yako uhai kwa maarifa sahihi.
Drag file here or click the button.