Kuhusu
Kreative Karakana

Kreative Karakana ni kampuni ya kidigitali inayojikita katika kuwawezesha wajasiriamali, vijana na wanawake kwa kuwapatia elimu, huduma na zana za biashara zinazokidhi mahitaji halisi ya soko la Tanzania na Afrika Mashariki. Tunatumia teknolojia, ubunifu na utafiti wa ndani kubuni suluhisho vinavyorahisisha uendeshaji wa biashara, kuongeza ufanisi, na kuwezesha ukuaji endelevu.

Katika safari yetu tangu mwaka 2021, tumekuwa tukijitofautisha kwa:

  • Kutoa huduma zinazolenga kuongeza thamani ya biashara ndogondogo na za kati.

  • Kujenga mifumo inayowezesha upatikanaji wa taarifa sahihi na mafunzo ya vitendo.

  • Kusimamia ubora, urahisi wa matumizi na usawa katika upatikanaji wa huduma kwa wajasiriamali wa ngazi zote.

  • Kufanya kazi kwa karibu na wadau mbalimbali ili kuimarisha mazingira ya biashara na kuongeza fursa za kiuchumi.

Kadri tunavyokua, ndivyo pia timu yetu inakua. Tunatafuta wataalamu wenye weledi, maadili ya kazi na uwezo wa kuchangia katika ujenzi wa suluhisho endelevu kwa biashara ndogo na za kati.

Ikiwa wewe ni Mhasibu Msaidizi mwenye umahiri, umakini wa hali ya juu na uwezo wa kufanya kazi kwa usahihi katika mazingira ya kitimu, ya kisasa na yanayokua kwa kasi, basi nafasi hii ni kwa ajili yako. Utakuwa sehemu ya timu inayohakikisha mifumo ya fedha inafanya kazi kwa ufanisi, rekodi zinatunzwa kwa umakini, na taarifa muhimu zinapatikana kwa wakati ili kusaidia maamuzi ya kimkakati.

Nafasi hii inafaa kwa mtu anayependa takwimu, anayethamini uwazi na maadili ya kazi, na mwenye shauku ya kukuza taaluma yake katika uhasibu ndani ya shirika linaloendelea kupanuka. Ikiwa unatafuta mahali pa kujenga uwezo, kukua kitaaluma na kufanya kazi yenye athari ya kweli Kreative Karakana ni sehemu sahihi.

Majukumu ya Kazi

Mhasibu Msaidizi atakuwa na jukumu la kusaidia idara ya fedha katika:

1. Usimamizi na Uhuishaji wa Rekodi za Kifedha

  • Kuingiza taarifa mpya kwenye vitabu vya hesabu au mifumo ya uhasibu.

  • Kuhakikisha taarifa zote mpya zinahifadhiwa na kurekebishwa ipasavyo.

2. Upatanisho wa Akaunti (Account Reconciliation)

  • Kufananisha taarifa za mapato na matumizi kati ya vitabu vya hesabu, benki, na kumbukumbu nyingine.

  • Kutambua tofauti, makosa, na kuyatatua kwa wakati.

3. Kuandaa Ripoti za Mapato na Matumizi

  • Kuandaa ripoti za kila wiki na kila mwezi.

  • Kuchambua mwenendo wa mapato na matumizi ili kusaidia uongozi kufanya maamuzi sahihi.

4. Ufuatiliaji wa Malipo, Ankara, na Risiti

  • Kufuatilia ankara zilizotumwa na zilizopokelewa.

  • Kuhakikisha malipo yote yanachakatwa ipasavyo na kwa wakati.

5. Kuandaa Nyaraka za Kodi na Taarifa za Kifedha

  • Kusaidia kuandaa nyaraka zinazohitajika na TRA.

  • Kuhakikisha kampuni inafuata taratibu zote za kikodi.

6. Kufanya Kazi kwa Uk closeu na Idara Nyingine

  • Kusaidia idara ya uendeshaji na uongozi kufuatilia matumizi.

  • Kuhakikisha matumizi yanaendana na bajeti ya kampuni.

7. Kufuatilia Uzingatiaji wa Kanuni na Taratibu za Kampuni

  • Kuhakikisha kampuni inafuata sera za fedha, kanuni, na mifumo iliyowekwa.

Jinsi ya kutuma Maombi

Waombaji wote wanapaswa kutuma barua ya maombi (cover letter) pamoja na CV kupitia barua pepe:
info@kreativekarakana.com

Muda wa mwisho kutuma maombi: 18/12/2025, saa 6 usiku.

Tafadhali kumbuka: Maombi yatakayowasilishwa baada ya muda huo hayatapokelewa wala kufanyiwa kazi.

Wote watakaofuzu mchujo wa kwanza watawasiliana nasi kabla ya tarehe 30/12/2025 kwa hatua inayofuata ya mchakato wa ajira.