Kuhusu
Kreative Karakana
Kreative Karakana ni kampuni ya kidigitali inayojikita katika kuwawezesha wajasiriamali, vijana na wanawake kwa kuwapatia elimu, huduma na zana za biashara zinazokidhi mahitaji halisi ya soko la Tanzania na Afrika Mashariki. Tunatumia teknolojia, ubunifu na utafiti wa ndani kubuni suluhisho vinavyorahisisha uendeshaji wa biashara, kuongeza ufanisi, na kuwezesha ukuaji endelevu.
Katika safari yetu tangu mwaka 2021, tumekuwa tukijitofautisha kwa:
Kutoa huduma zinazolenga kuongeza thamani ya biashara ndogondogo na za kati.
Kujenga mifumo inayowezesha upatikanaji wa taarifa sahihi na mafunzo ya vitendo.
Kusimamia ubora, urahisi wa matumizi na usawa katika upatikanaji wa huduma kwa wajasiriamali wa ngazi zote.
Kufanya kazi kwa karibu na wadau mbalimbali ili kuimarisha mazingira ya biashara na kuongeza fursa za kiuchumi.
Kadri tunavyokua, ndivyo pia timu yetu inakua. Tunatafuta wataalamu wenye weledi, maadili ya kazi na uwezo wa kuchangia katika ujenzi wa suluhisho endelevu kwa biashara ndogo na za kati.
Ikiwa wewe ni Afisa Uendeshaji mwenye umahiri, umakini wa hali ya juu na uwezo wa kuratibu kazi kwa ufanisi katika mazingira ya kitimu, ya kisasa na yanayokua kwa kasi, basi nafasi hii ni kwa ajili yako. Utakuwa sehemu ya timu inayohakikisha shughuli za kampuni zinaenda kwa mpangilio, mifumo inafanya kazi kwa ufanisi, taarifa muhimu zinawasilishwa kwa wakati, na kila idara inapata usaidizi unaohitajika ili kufikia malengo ya pamoja.
Nafasi hii inafaa kwa mtu anayependa kupanga na kuratibu shughuli, anayethamini uwazi na maadili ya kazi, na mwenye shauku ya kukuza taaluma yake katika uendeshaji ndani ya shirika linaloendelea kupanuka. Ikiwa unatafuta mahali pa kujenga uwezo, kukua kitaaluma na kufanya kazi yenye athari ya kweli, Kreative Karakana ni sehemu sahihi.
Majukumu ya Kazi
1. Uratibu na Usimamizi wa Shughuli za Kila Siku
Kufuatilia na kuhakikisha shughuli zote za kampuni zinafanyika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Kuratibu kazi kati ya idara mbalimbali: Learning, Digital Services, Marketing, na Tech.
Kufuatilia maombi na kazi za wateja kupitia mifumo yetu na kuhakikisha zinakamilika vizuri.
2. Uboreshaji wa Mifumo na Taratibu
Kubaini changamoto katika mifumo iliyopo na kupendekeza maboresho.
Kushirikiana na timu kuhakikisha taratibu za kazi zinafuatwa.
Kuandaa na kusimamia SOPs (Standard Operating Procedures).
3. Usimamizi wa Miradi (Project Coordination)
Kufuatilia maendeleo ya miradi, kuweka ratiba, na kuhakikisha timu inatimiza malengo.
Kuandaa ripoti za mradi na maendeleo ya kazi za kila wiki/mwezi.
Kufanya mawasiliano na wadau wa nje na wa ndani.
4. Huduma kwa Wateja na Mawasiliano
Kuhakikisha wateja wanapata mrejesho kwa wakati.
Kusimamia mfumo wa ticketing/requests za huduma.
Kupokea na kushughulikia changamoto za wateja na kutoa mrejesho kwa timu husika.
5. Uchambuzi na Utayarishaji wa Ripoti
Kuandaa ripoti za uendeshaji:
Idadi ya kozi zinazofanyika
Maendeleo ya wanafunzi
Maombi ya huduma
Kazi za freelancers
Kiwango cha mafanikio ya huduma
Kuchambua data na kupendekeza maamuzi ya kuboresha uendeshaji.
Jinsi ya kutuma Maombi
Waombaji wote wanapaswa kutuma barua ya maombi (cover letter) pamoja na CV kupitia barua pepe:
info@kreativekarakana.com
Muda wa mwisho kutuma maombi: 18/12/2025, saa 6 usiku.
Tafadhali kumbuka: Maombi yatakayowasilishwa baada ya muda huo hayatapokelewa wala kufanyiwa kazi.
Wote watakaofuzu mchujo wa kwanza watawasiliana nasi kabla ya tarehe 30/12/2025 kwa hatua inayofuata ya mchakato wa ajira.
